John 13:18-23

18 a“Sisemi hivi kuhusu ninyi nyote. Ninawajua wale niliowachagua. Lakini ni ili Andiko lipate kutimia, kwamba, ‘Yeye aliyekula chakula changu, ameinua kisigino chake dhidi yangu.’

19 b“Ninawaambia mambo haya kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa Mimi ndiye. 20 cAmin, amin nawaambia, yeyote anayempokea yule niliyemtuma anipokea mimi, naye anipokeaye mimi ampokea yeye aliyenituma mimi.”

Isa Anatabiri Kusalitiwa Kwake

(Mathayo 26:20-25; Marko 14:17-21; Luka 22:21-23)

21 dBaada ya kusema haya, Isa alifadhaika sana moyoni, akasema, “Amin, amin nawaambia, mmoja wenu atanisaliti.”

22Wanafunzi wake wakatazamana bila kujua kuwa alikuwa anamsema nani. 23 eMmoja wa wanafunzi wake ambaye Isa alimpenda sana, alikuwa ameegama kifuani mwa Isa.
Copyright information for SwhKC